Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bingwa mara mbili wa Olimpiki 'haoni aibu kuwa tofauti'

Bingwa Mara Mbili Wa Olimpiki 'haoni Aibu Kuwa Tofauti' Bingwa mara mbili wa Olimpiki 'haoni aibu kuwa tofauti'

Tue, 7 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Bingwa mara mbili wa Olimpiki Caster Semenya anasema "hataona aibu" kuwa "tofauti", na "atapigania kile ambacho ni sawa" huku kukiwa na mzozo unaoendelea na mamlaka ya riadha.

Semenya, 32, alizaliwa na tofauti za ukuaji wa kijinsia (DSD) na hawezi kushindana katika matukio ya wanawake bila kutumia dawa za kupunguza testosterone.

Mwafrika Kusini huyo anataka kuliwajibisha shirikisho la Riadha duniani kwa kile anachosema ni ubaguzi dhidi ya wanariadha wenye hyperandrogenism na hivi karibuni alisema anaelekeza mawazo yake kwenye "kushinda vita dhidi ya mamlaka" badala ya kukusanya medali, na kushiriki katika Olimpiki ya Paris 2024 tena.

Katika mahojiano mapana na Sally Nugent wa BBC Breakfast, Semenya anasema:

Alijiona "alikuwa tofauti" na umri wa miaka mitano lakini "anakumbatia" tofauti zake Hatapigania vita vya "kukubalika" Anataka kuwawezesha wanawake "kuwa na sauti" "Viongozi" katika michezo "wanawageuza wanawake dhidi ya wanawake" Hyperandrogenism ni hali ya kiafya inayoonyeshwa na viwango vya juu kuliko kawaida vya testosterone, homoni ambayo huongeza misuli na nguvu.

Chini ya kanuni zilizoanzishwa mwaka wa 2018, wanariadha walio na DSD waliruhusiwa tu kushindana katika mashindano ya mbio za wanawake kati ya mita 400 na maili ikiwa wangepunguza viwango vyao vya testosterone.

Mnamo Machi, Shirikisho la riadha Duniani liliamua kwamba wanariadha wa DSD lazima sasa wapate matibabu ya homoni hiyo kwa miezi sita kabla ya kuhitimu kushindana katika mashindano yote ya kike.

"Kwangu naamini kama wewe ni mwanamke, wewe ni mwanamke," alisema Semenya, ambaye alishinda dhahabu ya Olimpiki ya mita 800 mwaka wa 2012 na 2016 na ni bingwa wa dunia mara tatu wa mbio hizo .

"Haijalishi tofauti ulizonazo. Nimegundua nataka kuishi maisha yangu na kupigania kile ninachofikiria na ninajiamini.

"Najua mimi ni mwanamke na chochote kitakachoambatana nacho ukubali tu."

Semenya alikimbia mbio za mita 5,000 kwenye Mashindano ya Dunia ya mwaka jana huko Oregon lakini akashindwa kufuzu kwa fainali.

Mnamo Julai, Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu (ECHR) iliamua kumuunga mkono katika kesi inayohusiana na viwango vya testosterone kwa wanariadha wa kike.

Chanzo: Bbc