Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi apona kutekwa na Hamas baada ya kumtaja Messi

Bibi Hamas Bibi apona kutekwa na Hamas baada ya kumtaja Messi

Sat, 9 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwana Mama wa miaka 90 ameepuka kutekwa na kundi la Hamas baada ya kuwaambia kuwa ametoka nchi moja na Leonel Messi [Argentina].

Mzee huyo alisema kuwa baada ya wana kikundi hao kutaka kuwateka aliwauliza kama wanaangalia mpira na wakajibu huwa wanaangali kisha akawaeleza kuwa anatoka nchi moja na Messi.

Baada ya maelezo hayo Bibi huyo,mmoja wa wana kikundi cha Hamas alifurahi na kumshika bega, kisha kumwambia aonyeshe alama ya upendo na wakapiga picha ya pamoja na mwisho watekaji wakaondoka na kumuacha yeye na familia yake salama.

"Nilimuuliza, Unaangalia mpira ?, akasema anapenda na nikamwambia nimetoka nchi moja na Messi."

"Alishangaa sana na kuniambia kuwa anampenda sana Messi.Akawa ameweka mkono wake begani kwangu, akanipa bunduki yake na akaniambia nionyeshe ishara ya upendo na akapiga picha na mimi."

Mwana Mama huyo anayejulikana kwa jina la Esther Cunio ana uraia wa Argentina na Israel kidogo apelekwe Gaza pamoja na wanafamilia wengine nane [8] lakini baada ya kutaja jina la Messi hakutekwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live