Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara mtihani makundi CAF

Efb078cc64f0398f16eb450738564dc0.jpeg Biashara mtihani makundi CAF

Fri, 15 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

WAWAKILISHI wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika, Biashara United leo wataikabili Al Alhly Tripoli ya Libya kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa hatua ya kwanza kutafuta nafasi ya kucheza hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Biashara United watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Al Alhly Tripoli ambayo imetinga hatua hiyo baada ya kuibwaga Hay al Wadi ya Sudan kwa mabao 4-0.

Biashara United imeingia hatua hiyo baada ya kuiondoa FC Dikhil ya Djibouti kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda ugenini 1-0 na kushinda nyumbani 2-0 katika michezo ya awali.

Biashara United ni mara ya kwanza kushiriki michuano ya Afrika tangu ilipoanzishwa mwaka 1990, lakini hali ni tofauti kwa wapinzani wao wenye uzoefu wa kucheza michezo ya Kombe la Shirikisho.

Al Ahly Tripoli ilianza kucheza michuano ya kimataifa mwaka 2007 na iliishia hatua ya awali 2009, 2010 na 2014, mafanikio makubwa kupata ni mwaka 2016 ilipofika hatua ya makundi.

Akizungumza na HabariLEO jana, Kocha wa Biashara, Patrick Odhiambo alisema wanatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa wapinzani wao ambao mara ya mwisho kukutana nao ni mwaka mmoja uliopita katika mchezo wa kirafiki akiwa na Gor Mahia ya Kenya.

"Natarajia upinzani kutoka kwa wapinzani wangu ingawa maandalizi ya yamekamilika, wachezaji wangu wako tayari nimewaandaa kwa ajili ya mapambano kwani naufahamu ubora wa wapinzani,” alisema Odhiambo.

Alisema malengo yao ni kupata matokeo mazuri nyumbani ambayo yatawapa mwelekeo mzuri wa kwenda kutafuta matokeo mazuri zaidi ugenini ili kuvuka na kucheza hatua inayofuata.

Odhiambo alisema wanatarajia kupata upinzani mkali kwani wapinzani wao ni wazoefu, lakini wamejipanga kupata ushindi ingawa wataingia kwa tahadhari katika mchezo huo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz