Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara Utd hesabu kali kwa Yanga

90289 Yanga+pic Biashara Utd hesabu kali kwa Yanga

Tue, 31 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Wakati Biashara United ikijiandaa kuikabili Yanga kesho Jumatatu, kocha wa timu hiyo Francis Baraza amesema kuwa malengo yake ni kuendeleza rekodi ya ushindi katika mechi zake.

Biashara United imeonekana kuwa fiti tangu kutua kwa kocha huyo raia wa Kenya, ambaye alichukua mikoba ya Amri Said ‘Stam’ aliyesitishiwa mkataba kutokana na matokeo yasiyoridhisha.

Tangu ajiunge na timu hiyo ya mjini Musoma, Baraza ameiongoza katika mechi nne ikiwamo moja ya Kombe la Shirikisho, ambapo ameshinda tatu na sare moja.

Biashara United inatarajia kuumana na Yanga katika mwendelezo wa mechi za Ligi Kuu, mpambano ambao utapigwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Hadi sasa Biashara wamekusanya pointi 15 katika nafasi ya 15 baada ya kucheza mechi 13, huku Yanga wakiwa na alama 21 katika nafasi ya tatu baada ya mechi 10.

Akizungumza na Mwananchi, Baraza alisema licha ya kwamba ni mara yake ya kwanza kukutana na Yanga, lakini hilo kwake hajali kwani kila mchezo anaupa umuhimu kuhakikisha anaendeleza ushindi.

Alisema wataingia uwanjani kwa tahadhari na umakini na kwamba kwa maandalizi waliyoyafanya pamoja na morali ya wachezaji wake anaamini watapata pointi tatu na kujinasua nafasi za chini.

“Tunawaheshimu Yanga na tunaijua ni timu kubwa, lakini uwanjani tutakuwa na idadi sawa kwahiyo mimi ninachohitaji ni ushindi ili kujinasua nafasi za chini, kikosi changu kipo sawa,” alisema Mkenya huyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz