Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biashara United yamnasa Junior

28755 Pic+biashara TanzaniaWeb

Mon, 26 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Timu ya Biashara United ya mkoani Mara imemsajili mshambuliaji chipukizi Waziri Junior kwa mkopo kutoka Azam FC na tayari ameshaanza mazoezi na timu hiyo.

Timu hiyo inayocheza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya kwanza msimu huu pia inaendelea na mazugumzo ya kumsajili Innocent Edwin wa Mwadui FC pamoja na Kazungu Mashauri kutoka Singida United. Meneja wa Biashara, Amani Josia alisema wamepania kuwasajili wachezaji hao ili kuboresha safu ya ushambuliaji ambayo ilishindwa kufunga mabao ya kutosha katika michezo 13 waliyocheza mpaka sasa. Timu hiyo ndiyo iliyofunga mabao machache hadi sasa kwenye ligi kuu msimu ikiwa na mabao manne pekee na ndiyo inayoburuza mkia ikiwa na pointi kumi.

Hali hiyo imemkwaza kocha Hitimana Thierry raia wa Burundi, ambaye ameuomba uongozi kusajili washambuliaji wazoefu ili kuimarisha kikosi chake.

Josia alisema wameyafanyia kazi maombi ya kocha na anaamini watakamilisha usajili wa wachezaji hao wote na kuiwezesha timu yao kufanya vema katika medchi zijazo na kuweza kuiondoa timu kutoka mkiani na kupanda katika nafasi za juu.



Chanzo: mwananchi.co.tz