Mshambuliaji wa Simba, Benard Morrison amejitokeza kuishukuru Klabu ya Yanga kwa kumpa heshima ya kuichezea timu hiyo kabla ya kutimkia Simba ambapo safari yake ilizua utata kiasi cha kufunguliwa kwa kesi katika mahakama za michezo.
Kupitia mitandao ya kijamiiĀ Benard Morrison ameandika haya ikiwa ni siku mojaa baada ya kushinda kesi iliyokuwa ikiunguruma katika Mahakama ya usuluhishi michezoni CAS.
'Kuna mwanzo na mwisho wa kila jambo,hakuna jambo linalodumu milele.'' ''Sote tumekuwa tukingojea hukumu hii( Kwa majibu mazuri au mabaya).
Hatimaye imemalizika na kufuta mashaka na mivutano yote iliyokuwepo.'' ''Nataka kila mtu ajue jinsi ninavyoithamini yanga kwa nafasi waliyonipa kuwawakilisha na kuvaa nembo yao.''
''Hakuna hata mmoja hapa Tanzania alinijua au kujali kazi yangu hadi Luc Aymael aliponileta kucheza hapa.'' ''Asante kocha kwa kuniamini na kunifanya kuwa mkubwa.
Kuna msemo huko Ghana unasema '' daktari mbaya aliyekuhudumia mpaka daktari mzuri alipofika inabidi naye ashukuriwe.'' ''Hata kama ilikuwa ni mbaya, alikuhifadhi na kukuhudumia mpaka mazuri yalipokufikia.''
''Hii ni rasmi kusema asante Yanga na yeyote aliyenifanya nitabasamu.'' Siwezi kusahau upendo nilioonyeshwa na mashabiki wao.