Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki wa zamani wa Yanga awalilia wadau

68617 Pic+yanga

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

UNAMKUMBUKA Allan Shomari, mmoja ya mabeki wa kati mahiri waliowahi kuibuka na kutamba nchini miaka ya 1970-1980? Basi jamaa huyo amepatwa na mtihani wa kupofuka macho kwa muda mrefu na kumkwamisha shughuli zake za kila siku.

Sasa unaambiwa mapema leo asubuhi beki huyo ambaye alipoteza uoni wake tangu mwaka 2007 amewaliliwa wadau mbalimbali wa soka kwa kuwaomba wamsaidie kupata matibabu yake ya tatizo lake hilo, ili arejeshwe na uwezo wake wa kuona na kufanya yake.

Shomari aliyekuwa msaada mkubwa ndani ya Yanga na Taifa Stars enzi akikipiga alitoa rai yake hiyo yasema ha ambae alikuwa msaada mkubwa pia katika kikosi cha timu ya Taifa miaka ya 80, ameyasema hayo nyumbani kwake Kisongo jijini Arusha alipotembelewa na wanachama wa klabu hiyo tawi la Arusha katika kuadhimisha Wiki ya Mwananchi.

Shomari amesema amecheza mpira tangu miaka ya 1970, katika timu mbali mbali za Arusha na baadae kuichezea Yanga mwaka 1981 kabla ya kustaafu mwaka 1987.

"Baada ya kuachwa katika kikosi cha kwanza mwaka huo nikaacha soka na kuajiriwa katika mabasi kama dereva lakini mwaka 2006 nilianza kupata uhafifu wa kuona kabla ya 2007 macho kuzima kabisa," amesema kwa masikitiko.

Amesema licha ya kuhangaika kwa matibabu ya kawaida kwa muda mrefu hajafanikiwa kupata tiba hadi aliposhauriwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kumenywa ngozi ya juu ya mboni ili aweze kuona tena.

Pia Soma

"Yaani jamani natamani sana kuona, natamani zaidi watu wengine wanavyofikia lakini uwezo wa kusafiri nje ya nchi tu siwezi, licha ya kujigharamia matibabu huko hivyo niombe watu wajitokeze kunisaida angalau nisife nikiwa kipofu."

Mwenyekiti wa matawi ya Yanga Arusha, Felician Mombo amesema hali ya Shomari inaumiza na kuahidi watajitahidi kumjulia hali na kumfariji Shomari ambae alikuwa mpiganaji katika kikosi chao.

"Katika siku hizi za kuadhimisha Wiki ya Mwananchi, tunafanya huduma mbali mbali za kijamii na kuwatembelea wachezaji wetu waliowahi kuichezea timu yetu wakapata matatizo ambapo leo tumechanga vitu mbali mbali ikiwemo sukari, unga, mchele, mafuta, nguo, sabuni na vingine vingi na kumletea kama kumfariji," alisema.

Mbali na Shomari wanachama hao pia walitembelea kituo cha watoto Yatima cha Karimu kilichoko Muriet ambapo waliwapa msaada ya vitu mbali mbali.

Mkurugenzi wa Kituo hicho, Rehema Kindoi alishukuru kwa msaada huo aliosema kituoni kwake kuna jumla ya watoto 24 kati ya 20 wanasoma shule mbalimbali na wengine wakiwa ni  wadogo akiwem wa miezi mitatu aliyetelekezwa Hospital ya St Elizabeth.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz