Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki wa Ivory Coast afanyiwa vipimo Simba

29433 Vipimo+pic TanzaniaWeb

Fri, 30 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Beki wa kimataifa wa Ivory Coast, Coulibaly Zana amefanyiwa vipimo vya afya mchana wa leo Alhamisi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Zana aliwasili nchini jana Jumatano kwa ajili ya kukamilisha usajili wake na Simba anachosubiri sasa ni kusaini mkataba na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu nchini.

Zana aliwasili Muhimbili saa 7:54 mchana akiwa na daktari wa timu hiyo Yassin Gembe na moja kwa moja kuanza taratibu za vipimo vyake.

Mwanaspoti online ilikuwa imepiga kambi Muhimbili ilishuhudia zoezi zima la beki huyo akifanyiwa vipimo na daktari wa kitengo cha moyo, Dr George Longopa.

Mchezaji huyo alionekana kuwa fiti katika zoezi la utimamu wa moyo ambalo alilifanya vyema katika dakika zote alizopangiwa.

Taarifa za awali ambazo Mwanaspoti imeshuhudia ni kwamba Zana ana asilimia kubwa ya kufuzu vipimo hivyo baada ya kuhimili zoezi hilo lenye kutambua kwa kiwango kikubwa jinsi moyo unavyoweza kuhimiliki mikikimikiki yote ya uwanjani.

Zana amekuja kuziba pengo la Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi na atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya miezi miwili.

Beki huyo imedaiwa atasaini mkataba muda wowote kuanzia sasa baada ya vipimo hivyo na kuanza kazi ndani ya Simba.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz