Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Prisons amfunda kipa Yanga

8928 BEKI+PIC TZW

Tue, 12 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Beki wa Tanzania Prisons, Salum Kimenya, amemtaka kipa wa Yanga, Beno Kakolanya kufanya uamuzi sahihi katika dirisha la usajili.

Akizungumza na gazeti hili, Kimenya alimtaka Kakolanya kuangalia klabu bora ambayo atakwenda kupata nafasi ya kucheza.

“Hakuwa na wakati mzuri Yanga, lakini kama kuna timu zinamtaka ni muda wake wa kuamua nini cha kufanya, kama ataondoka aende sehemu ambayo atapata nafasi ili kurejesha kiwango chake,” alisema Kimenya.

Mchezaji huyo alidai Kakonya ana nafasi ya kurejesha makali yake akipona vyema majeraha ambayo yalimuweka nje ya uwanja muda mrefu.

“Tulicheza pamoja Prisons naamini kama atapona msimu ujao atakuwa Kakolanya wa tofauti, umri wake sio mkubwa lakini ni mtu asiyeyumba katika kusimamia uamuzi wake,” alisema.

Licha dirisha la usajili kutofunguliwa, klabu za Ligi Kuu Tanzania zinapigana kumbo kuwania saini za wachezaji mbalimbali ili kuboresha timu zao.

Chanzo: mwananchi.co.tz