Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Beki Mwadui atangaza hawaogopi Simba

Wed, 6 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

BEKI wa kati wa Mwadui FC, Revocatus Mgunga amesema kuwa ataingia uwanjani bila hofu wala woga katika kumkabili Straika wa Simba, John Bocco pindi timu hizo zitakapokutana dimbani na hatarajii kutokea tukio lolote kesho Alhamisi.

Timu hizo zinakutana katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam,huku wawili hao wakikumbuka matukio tofauti haswa ya kugongana uwanjani ikiwa ni misimu miwili mfululizo.

Katika mechi ya mwisho iliyopigwa Septemba 23 mwaka jana katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga ilisababisha Bocco kutolewa kwa kadi nyekundu na kukumbana na adhabu ya kusimamishwa michezo mitatu na faini ya Sh 500,000 kwa kumpiga ngumi beki huyo.

 

Akizungumza na Mwanaspoti,Mgunga alisema kuwa ataingia uwanjani kwa umakini na kujiamini na kwamba hatamuogopa Straika huyo badala yake atafanya kazi yake na hatarajii kutokea tena tukio lolote.

Alisema kuwa amejiandaa vizuri kutimiza majukumu yake ya uwanjani na matarajio yake ni kuisaidia timu kupata matokeo mazuri ambayo yataiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa Ligi kuu.

“Kwanini nimuogope mwanadamu mwenzangu? Nitaingia uwanjani kwa umakini na kujiamini kuhakikisha natimiza majukumu yangu na kupata matokeo mazuri kwa faida ya timu yangu”alisema Mgunga.

Beki huyo aliongeza kuwa hata hivyo wanajitupa dimbani leo wakihitaji kulipa kisasi kwani katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wakiwa uwanjani wa nyumbani mjini Shinyanga walipoteza kwa mabao 3-1.

Alieleza kuwa bado Mwadui hawapo nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi,hivyo kipaumbele chao leo ni kuhakikisha wanavuna alama tatu na kupanda nafasi za juu na kwamba hawawaogopi wapinzani wao.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz