Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bayi ataja chanzo rekodi yake kutovunjwa miaka 57

Bayi Pic Data Bayi ataja chanzo rekodi yake kutovunjwa miaka 57

Thu, 11 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroMore by this Author WAKATI kesho Alhamis Machi 11, rekodi za dunia za Mtanzania, Filbert Bayi zikitarajiwa kuingizwa kwenye jumba la makumbusho ya riadha ya dunia, nyota huyo wa mbio za kati ametaja sababu zilizochangia rekodi yake kutovunjwa kwa miaka 57.

Bayi alivunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 1500 kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola ya 1974 huko Christchurch huko Newzealand, akichuana na Ben Jipcho wa Kenya, John Walker aliyekuwa nyumbani na Rod Dickson aliyekuwa mshindi wa medali ya shaba ya Olimpiki ya 1972.

Mwanariadha huyo alitumia dakika 3:51:00 kumaliza mbio hizo na kuvunja rekodi ya dunia ya dakika 3:51:01, rekodi ambayo haijavunjwa hadi leo kwenye michezo ya Jumuiya ya Madola.

"Tuliovunja rekodi ya dunia ya mbio za mita 1500 na maili moja hatuvuki 15 duniani, japo wapo wengine waliovunja rekodi za mbio mbalimbali," anasema Bayi na kuongeza kwamba.

"Zamani tulikimbia kwa ridhaa, huenda ndiyo sababu tulijitoa sana, leo hii vijana wengi wanakimbia sababu ya pesa na kwenye michezo ya Jumuiya Madola hakuna pesa.

"Hivyo wengi wao wanashindwa kujitoa muhanga na kuumia kwenye mbio ambayo haina pesa ili mradi tu avunje rekodi, hii ndiyo sababu kubwa ambayo rekodi yangu imeshindwa kuvunjwa hadi sasa katika michezo ya Madola," anasema Bayi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz