Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barcelona, Madrid kufuana leo

03b686730999a503156392b124ca1067 Barcelona, Madrid kufuana leo

Sat, 24 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VIGOGO wawili wa soka nchini Hispania Barcelona na Real Madridi leo hii wanakutana katika mchezo wa El Classico, utakaopigwa Camp Nou, majira ya saa 11 jioni.

Mchezo wa mwisho Barca alipoteza kwa mabao 2-0. Wakati wachezaji Vinicius Junior na Mariano Diaz wakiibuka mashujaa wa mchezo huo kwa kupachika mabao hayo. Msimamo wa La Liga unaonyesha Real Madrid inashika nafasi ya tatu ikiwa na alama 10 na Barcelona iko nafasi ya 10 akiwa na pointi saba.

Rekodi

Rekodi zinaonyesha kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita, Barca ameshinda mara nyingi zaidi (16) dhidi ya (11) za Madrid. Huku michezo 10 ikimalizika kwa sare.

Zaidi ya mabao 118 yamegusa nyavu za mahasimu hawa, Barcelona akipachika mabao 67 na Madrid 51. Lionel Messi anaongoza kwa kufunga mabao 19, akifuatiwa na Cristiano Ronaldo mwenye mabao 18 ,Suarez aliyehamia Atletico Madrid akiwa na 11.

Chanzo: habarileo.co.tz