Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Barca, Boca Juniors kumkumbuka Maradona

Ed721bbd6d8c22fdc7b1de2ffa508e34.png Barca, Boca Juniors kumkumbuka Maradona

Wed, 27 Oct 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KLABU ya La Liga ya Barcelona itacheza na miamba ya Argentina Boca Juniors Desemba mwaka huu kukumbuka mwaka mmoja wa kifo cha mchezaji wa kimataifa wa zamani wa Argentina, Diego Maradona.

Klabu hizo zilitangaza jana kuwa: “FC Barcelona na klabu Atletico Boca Juniors tutacheza Kombe la Maradona Desemba 14, mechi ya kumbukumbu ya mwaka mmoja wa kifo cha nyota Diego Armando Maradona.”

Boca imethibitisha kucheza mechi hiyo pia ikisema itachezwa Mrsool Park Riyadh, Saudi Arabia. Maradona alifariki kwa ugonjwa wa shambulio la moyo Nobemba 25, mwaka jana baada ya kufanyiwa upasuaji.

Wakati wa uhai wake, Muargentina huyo alicheza Barca na Boca katika historia yake ya soka na kote alipata mafanikio makubwa ikiwamo kubeba makombe.

Mafanikio yake makubwa zaidi katika ngazi ya klabu aliyapata akiwa na Napoli ya Italia. Pia aliiongoza Argentina kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1986 lilipofanyika Mexico.

Chanzo: www.habarileo.co.tz