Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Banda alivyoacha deni kwa Samatta, Msuva, Kichuya

10349 Pic+banda TanzaniaWeb

Mon, 6 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Soka ni miongoni mwa michezo inayotumia zaidi nguvu, akili, maarifa na ili mchezaji acheze kwa kiwango bora, anapaswa kuwa na utimamu wa mwili.

Baadhi ya wachezaji waliwahi kupata madhara na kuweka rehani vipaji vyao kwa kushindwa kutunza utimamu wa mwili na mmoja wa nyota hao ni Kevin Prince Boateng.

Mfungaji bora wa muda wote wa mabao Arsenal, Thierry Henry, aliwahi kukaririwa akisema nusura ndoa yake ihitimishe safari ya soka baada ya kuachana na mkewe.

Baada ya kudumu katika ndoa kwa miaka minne, Claire Merry, aliomba talaka mahakamani baada ya kushindwa kumaliza matatizo yao ya ndani.

Henry aliyelazimika kumlipa Claire Pauni8 milioni, anasema alipata mshituko uliompa msongo wa mawazo na moja ya sababu za kuihama Arsenal kwenda Barcelona ilikuwa kwenda kutuliza akili.

Hatari ya kutotunza mwili kunamfanya mchezaji kupata majeraha ya mara kwa mara, kuchoka haraka na wakati mwingine mchezaji anashindwa kuendelea na mchezo kutokana na uchovu.

Beki nguli wa Azam Aggrey Morris anasema siri kubwa ya kucheza muda mrefu kwenye kiwango bora inachangiwa na mkewe.

Mkasa wa Boateng ni fundisho kwa wachezaji wengine duniani wanaopenda starehe.

Boateng amekuwa akipenda kutumia mwili vibaya na mke wake, Melissa Satta amekuwa akilalamikia matukio ya mara kwa mara kuhusu mwenendo mbaya wa mchezaji huyo.

Matokeo ya kupenda starehe yalizalisha majeraha ya mara kwa mara ambayo yalimfanya kutimka AC Milan, baada ya kupoteza namba kwenye kikosi cha kwanza.

Wiki iliyopita mchezaji wa kimataifa anayecheza soka ya kulipwa Afrika Kusini, Abdi Banda, ameamua kuchukua ‘jiko’, baada ya kufunga ndoa na Zabibu Kiba.

Baada ya Banda anayecheza klabu ya Baroka ya Afrika Kusini, sasa ameacha deni kwa baadhi ya nyota hawa wa Tanzania ambao bado hawajaingia kwenye maisha ya ndoa.

SAIMON MSUVA

Mshambuliaji wa Difaa El Jadida ya Morocco, Saimon Msuva bado hajafunga pingu za maisha, nyota huyo za zamani wa Yanga ni miongoni mwa wachezaji waliotoa pongezi kwa Banda.

Akizungumzia mustakabali wake wa ndoa, Msuva anasema muda haujafika na utakapofika hatasita kufanya uamuzi wa kuachana na ukapera.

MBWANA SAMATTA

Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta anayecheza KRC Genk naye ameachiwa deni na Banda ambalo anatakiwa kulilipa ili kufanikisha mipango ya kupata mafanikio katika mchezo wa soka.

SHIZA KICHUYA

Licha ya Kichuya wa Simba kuachwa mbali kiumri na mastaa wenzake akina Samatta na Msuva, pia anatakiwa kuanza kuwa na mikakati ya kujiandaa kuingia kwenye maisha ya ndoa ili kulinda kipaji chake kwa kutochosha mwili wake.

HASSAN KESSY

Nyota wa zamani wa Yanga, Hassani Kessy aliyejiunga na Nkana FC ya Zambia ni miongoni mwa wachezaji walioachiwa deni na Banda, beki huyo wa kulia bado ‘anaseti’ mipango yake sawa kabla ya kuingia kwenye ndoa.

JONAS MKUDE

Kiungo wa Simba, Jonas Mkude hajaingia kwenye maisha ya ndoa ambayo Morris anaamini yanaweza kumsaidia mchezaji kutulia na kuwa kwenye kiwango bora muda mrefu.

Chanzo: mwananchi.co.tz