Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baba aiambia Mahakama “Naomba dakika 5 nifungiwe na shetani”

2532 Larry 660x400

Sat, 3 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Baba wa mabinti watatu waliodhalilishwa kingono na Daktari wa Mazoezi wa Marekani, Larry Nassar amejaribu kumshambulia mbele ya mahakama ya Michigan, baada ya kumvaa mshtakiwa huyo anayetuhumiwa kudhalilisha wachezaji kadhaa waliopitia mikononi mwake.

Hata hivyo Randall Margraves hakufanikisha lengo lake hilo baada ya kudhibitiwa vyema na maofisa watatu wa mahakamani hapo. Kabla ya kuvamia meza ya mshtakiwa Nassar, mwanaume huyo aliomba kupewa “dakika tano ili afungiwe na shetani huyo” Jaji Janice Cunningham akasema hawezi kuruhusu jambo hilo.

Lakini Margraves aliendelea kusisitiza apewe dakika moja na kusababisha vicheko vya chini chini kutoka chumba cha mahakama. Nassar, aliyewahi kuwa Daktari wa mazoezi wa Timu ya Olympiki ya Marekani, alishahukumiwa miaka 175 jela wiki iliyopita baada ya kutolewa ushahidi wa takribani waathirika 160 waliofanyiwa vitendo vya udhalilishaji kingono.



Akiwakilisha hukumu hiyo, Jaji Rosemarie Aquilina alimwambia Nassar: ” wewe hustahili kuonekana tena nje ya jela.”

Waathirika wengi ni wale waliochukuliwa kwaajili ya kutibiwa naye katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Michigan, alipokuwa akifanya kazi kama Daktari wa michezo.





 

MAZISHI JUMATATU: BADO HAIJULIKANI NI DINI GANI ITAMZIKA MZEE KINGUNGE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Chanzo: millardayo.com