Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Baada ya kutupia‘hat-trick’ Bale ajipanga kutwaa ubingwa dhidi ya Uruguay

5335 670951 Bale Wales Reuters 970 TZW

Mon, 26 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Wales, Gareth Bale amesema kuwa kushinda taji lake la kwanza dhidi ya timu yake ya taifa ya Wales ni kitu kikubwa zaidi kwake.



Bale ameyasema hayo baada ya hapo jana kuipatia hat-trick timu yake ya taifa ya Wales wakati ilipo chomoza na ushindi wa mabao 6 – 0 dhidi ya China kwenye mchezo wa michuano ya kombe la China Cup.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amesema kuwa kuipatia ubingwa Wales ni kitukikubwa zaidi kuliko hata kwa ngazi ya klabu.

Kushinda taji lolote huwa siku zote ni kitu kizuri lakini kuipatia timu yako ya taifa ni vizuri zaidi.

Ni jambo kubwa mno kwakuwa unafanya hivyo kutoka ndani ya moyo na ndani ya damu yako kwakua unataka kuifanya nchi yako ijivunie.

Kwa hiyo pengine liwe taji kama hili ambalo tunawania ama la bara la Ulaya na hatakama liwe lile la kombe la dunia siku zote raha ni kushinda taji.

Baada ya kuwatoa wenyeji China katika michuano hiyo ya China Cup sasa Wales watakutana na timu ya taifa ya Uruguay siku ya Jumatatu kwenye mchezo wa fainali.

Baada ya kutupia mabao hayo matatu (hat-trick) hapo jana yanamfanya kuweka rekodi yakuwa mfungaji wa muda wote ndani ya Wales kwakuwa na jumla ya mabao 29 ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na  Ryan Giggs.

Chanzo: bongo5.com