Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

BMT yatoa wito kwa vyama, mashirikisho

Image 365 1080x640.png Michezo BMT yatoa wito kwa vyama, mashirikisho

Thu, 11 May 2023 Chanzo: Dar24

Uongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), kupitia kwa Katibu Mtendaji, Neema Msitha, umevitaka Vyama na Mashirikisho ya michezo nchini kuhakikisha wanafanya tathimini ya kina ya ubora wa maandalizi yao kabla ya kwenda kushiriki kimataifa.

Msitha amesema: “Kumekuwa na kasumba ya baadhi ya vyama kwenda kushiriki mashindano ya kimataifa kwa kuwa tu wamepata mialiko bila kujali utayari wa timu zao kiushindani.

“Matokeo yake hujikuta wakifanya vibaya katika mashindano hayo na kuliaibisha Taifa, hivyo tunaviagiza vyama na Mashirikisho kufanya tathimini ya kina ya ubora wao kiushindani kabla ya kuthibitisha ushiriki wao kimataifa.”

Wakati huo huo Uongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), umeweka wazi kuwa mpango mkakati wa Shirikisho hilo kwa sasa ni kuhakikisha wanakuwa na mashindano mengi ya vijana kulingana na maagizo ya Shirikisho la Riadha Duniani.

Kama sehemu ya utekelezaji wa mpango mkakati huo, RT wanaendelea na maandalizi ya mashindano ya vijana chini ya miaka 14 ambayo yatafanyika kwa siku mbili, yaani keshokutwa Jumamosi na Jumapili.

Afisa Habari wa RT Lwiza John amesema: “Rais wa Shirikisho Riadha Duniani Sebastian Coe aliagiza mshirikisho wanachama kuhakikisha kunafanyika uwekezaji mkubwa kwa vijana na katika kutekeleza hilo nasi tunaendelea na maandalizi ya mashindano mbalimbali ya vijana.”

Chanzo: Dar24