Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA), limekabidhi uwanja wa mchezo wa kikapu kwa Chuo cha Ualimu Kawaida (TTC) na vifaa vya michezo kwa chuo chuo cha Ualimu Ufundi Mtwara vilivyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA), limekabidhi uwanja wa mchezo wa kikapu kwa Chuo cha Ualimu Kawaida (TTC) na vifaa vya michezo kwa chuo chuo cha Ualimu Ufundi Mtwara vilivyopo Manispaa ya Mtwara Mikindani. Mwenyekiti wa BAMMATA Brigedia Generali Selemani Gwaya amesema wametoa vifaa hivyo kwa vyuo hivyo viwili kwa kuwa vimeonesha uungwana katika kipindi chote cha michezo ya majeshi ambayo imefanyika kwa mafanikio makubwa.