Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yawaita Simba mezani saini ya Yakubu

50436 YAKUB+PIC

Thu, 4 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

SIMBA inamtolea macho beki flani mbishi na mwenye akili nyingi akiwa uwanjani Yakubu Mohammed wa Azam FC, lakini klabu yake inacheka baada ya kusikia taarifa hiyo kisha ikawaambia Wekundu wa Msimbazi kama wanamtaka Mghana huyo, basi waende Mzizima wakamalize kazi.

Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin ‘Popat’ ameliambia Mwanaspoti kuwa kama Simba inamuhitaji beki huyo kazi rahisi ni kuifuata Azam FC na kufungua mazungumzo ya dili hilo na watapewa bei na wakifika, basi freshi tu.

“Kama kweli Simba wanamtaka Yakubu, Azam tunawaita mezani tuzungumze na tutawapa bei halisi na wakiweza, basi wataondoka naye. Yakubu yupo hapa Azam,” alisema Popat.

Alisema Simba haiwezi kumpata bure Yakubu kwa kuwa licha ya kuwa kwenye mazungumzo ya kumuongezea mkataba, lakini uliopo kwa sasa bado haujaisha hadi Novemba, mwaka huu na uwezekano wa kumpata dirisha lijalo la usajili ni mdogo sana.

“Kama (Simba) wanamtaka Yakubu bure, basi wasubiri hadi Novemba ili wamchukue kwa sasa bado yuko ndani ya mkataba na Azam,” alisema Popat.

Bosi huyo aliongeza kuwa wanafuatililia ili kufahamu kama Simba inafanya mazungumzo ya siri na beki huyo kwa kuwa ni kosa na ikibainika hilo linafanyika bila ruhusu, basi watachukua hatua.

“Tuko katika mazungumzo na Yakubu kuhusu mkataba mpya na mambo yanakwenda vizuri hivyo, tunasubiri upande wake tu,” aliongeza.

Ana dili kubwa Misri

Wakati Azam wakisema hivyo taarifa kutoka Misri zinasema beki huyo ana ofa ya maana Misri na hicho ndicho kinachompa wakati mgumu kuongeza mkataba mpya.

Rafiki wa karibu wa Yakubu ameliambia Mwanaspoti kuwa, kinachompa ugumu beki huyo kusalia Azam ni mshahara mnono ambao Waarabu hao wanataka kumpa.



Chanzo: mwananchi.co.tz