Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yatuliza mashabiki, yaipania Namungo

78571 Pic+azam

Mon, 7 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIKOSI cha Azam FC usiku wa leo JUmamosi kinatarajiwa kuikaribisha Namungo FC ya Lindi, huku viongozi wa klabu hiyo wakiwatuliza mashabiki wakiwaambia watulie kwani mambo yatanyooka na watapata raha waitakayo.

Mashabiki wachache wa klabu hiyo wameanza kumkatia tamaa kocha wao, Etienne Ndayiragije baada ya kusuasa kwenye michuano inayoshiriki ikiwemo kung'olewa Kombe la Shirikisho Afrika na kushindwa kwa mbinde katika Ligi Kuu.

Azam ilitupwa nje ya Triangle United kwa jumla ya mabao 2-0, huku wakishinda KMC kwa mbinde bao 1-0 na kuinyuka Ndanda mabao 2-0, lakini mashabiki wakionekana kutoridhishwa na soka linalochezwa na timu yao nma kuanzisha zomea zomea wakimtaka Ndariragije atimke zake kikosini hapo.

Hata hivyo, klabu hiyo kupitia Ofisa Habari wa Azam, Jafar Idd alisema anawaomba mashabiki wa Azam wawe kitu kimoja na kumuunga mkono mwalimu.

"Tusapoti wachezaji, tuwasapoti viongozi, tunawakaribisha uwanjani na tumejiandaa kuondoka na ushindi katika mchezo huu," alisema.

Jafar alisema katika mchezo huo hakuna majeruhi kutokana na kutokuwa na majeruhi yoyote, hivyo mwalimu atakuwa na uwanja mpana wa kutanua kikosi chake.

"Maandalizi yameenda vizuri, mchezo uliopita tulicheza mpira wa kupendeza na tunatarajia kuuona mchezo mzuri dhidi ya Namungo," aliongea Jafar.

Azam inatarajiwa kushuka kwenye Uwanja wa Azam Complex, kuikaribish Namungo katika mechi itakayoanza saa 1 usiku, ikisaka alama nyingine tatu za kuwatoa eneo la katikati kuelekea eneo la juu linaloongozwa na watetezi Simba.

Simba inaongoza msimamo kwa sasa kwa alama 12, kikifuatiwa na Kagera Suhar yenye pointi 9, huku Lipuli, Tanzania Prisons na Ruvu Shooting zikifuata kwa pointi 8 kila mbele ya Namungo waliokusanya alama 7 katika mechi tano.

Chanzo: mwananchi.co.tz