Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yapitisha fagio la chuma, yatema wanne

Fagio Pic Data Azam yapitisha fagio la chuma, yatema wanne

Sun, 25 Jul 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Uongozi wa Azam FC umethibitisha kufikia makubaliana ya pande mbili ya kuachana na wachezaji wanne wa kimatiafa ambao ni beki wa kati, Yakubu Mohammed, kiungo Ally Niyonzima, mshambuliaji Mpiana Monzinzi na Obrey Chirwa ambaye mkataba wake umemalizika.

Taarifa iliyotolewa na Klabu hiyo inasema kuwa " Tumefikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na wachezaji wetu wanne wa kimataifa' Wachezaji hao ni beki wa kati, Yakubu Mohammed, kiungo Ally Niyonzima, mshambuliaji Mpiana Monzinzi na Obrey Chirwa, ambaye mkataba wake umemalizika"

"Azam FC tunawashukuru kwa mchango wao waliotoa katika klabu hii bora kipindi chote walichokuwa nasi na tunawatakia kila la kheri huko waendako"

kuondoka kwa wachezaji hao ni kutokana na kutokuwa na msimu mzuri tangu wajiungea na matajiri hao wa Jiji la Dar es Salaam hivyo kupisha wachezaji wengine wapya waliosajiliwa klabuni hapo ambao ni mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Rodgers Kola, kwa usajili huru akitokea Zanaco, Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia na Cape Town City ya Afrika ya Kusini Charles Zulu.

wengine ni beki kisiki wa kushoto wa kimataifa wa Tanzania, Edward Manyama kwa usajili huru akitokea Ruvu Shooting, kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Kenneth Muguna akitokea Gor Mahia ya Kenya na kiungo mkabaji wa kimataifa wa Zambia, Paul Katema, aliyetokea Red Arrows ya Zambia.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz