Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yapania kujifuta machozi Ligi Kuu Bara

1684 AZAM FC 243578 Azam yapania kujifuta machozi Ligi Kuu Bara

Mon, 13 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, amesema wamedhamiria kuhakikisha wanamaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, ili kuweka heshima.

Kauli hiyo ya Cioaba imekuja baada ya timu yake kuvuliwa ubingwa wa mashindano ya Kombe la FA, na hivyo kupoteza tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Cioaba alisema anaendelea kuimarisha mikakati ili kikosi chake kifanye vema katika mechi zilizobakia licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji wake nyota wa kikosi cha kwanza.

Cioaba alisema baada ya kutolewa katika mashindano ya Kombe la FA, nguvu zao zimeelekea katika kulinda heshima yao katika ligi hiyo ambayo mwakani itashirikisha timu 16 tu.

"Tumepoteza nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa, hali hiyo haitaturudisha nyuma kupambana kutafuta alama tatu katika mechi zetu zote zilizobaki, wachezaji wanalifahamu hilo, tutapambana timu kutafuta matokeo mazuri," alisema Cioaba.

Aliongeza anafahamu hakuna mechi rahisi kwa sababu kila timu inahitaji kutimiza malengo yake, huku vita kubwa ikiwa kwenye klabu zinazopambana kujinasua na janga la kushuka daraja.

"Wachezaji wanatakiwa kujituma kwa sababu hatujafikia malengo yetu, vijana wangu walicheza vizuri dhidi ya Mwadui FC, matokeo yake yametuimarisha na tunataka kuendeleza kasi ile," aliongeza kocha huyo.

Azam ina pointi 65 na iko katika nafasi ya pili kwenye msimamo nyumba ya mabingwa Simba yenye pointi 81, huku Yanga ikishinda nafasi ya tatu, huku kila timu ikibakiwa na mechi nne ili kumaliza msimu 2019/20.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live