Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam yaanza kutetea ubingwa Mapinduzi

34542 Pic+azam Tanzania Web Photo

Wed, 2 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Simba na Yanga zikiondoka leo kwenda Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi, bingwa Mtetezi wa Kombe la Mapinduzi, Azam inaingia uwanjani kucheza na Jamhuri kwenye Uwanja wa Amaan.

Azam ambayo iko Visiwani Zanzibar tangu juzi Jumatatu itafungua dimba kutetea ubingwa wake huo kwa mchezo utakaoanza saa 2:15 usiku.

Yanga iliyopeleka kikosi B, itarusha karata yao ya kwanza kesho Alhamisi dhidi ya KVZ huku watani zao, Simba wakitarajiwa kutupa kete ya kwanza Ijumaa itakapocheza na Chipukizi, mechi zote zitachezwa kwenye uwanja wa Amaan.

Kocha msaidizi wa Azam, Iddi Cheche alisema jana kuwa wamejipanga kutetea ubingwa wao ili kuweka rekodi ya kutwaa taji hilo kwa mara ya tatu mfululizo msimu huu.

“Timu iko vizuri, tuko Zanzibar tangu Jumatatu iliyopita kwa ajili ya mashindano haya, wachezaji wako vizuri, wana morali ya kutosha na bila shaka tutaendeleza rekodi ya ubingwa,” alisema.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema jukumu zima la timu Zanzibar anamwachia msaidizi wake, Noel Mwandila kwani yeye anaiandaa Yanga kwa ajili ya ubingwa.

“Tuko tayari kupambana, tunajiamini na tunaamini tutafanya vizuri pia kama ambavyo timu yetu imekuwa ikifanya kwenye Ligi Kuu,” alisema Zahera.

Mashindano hayo ambayo ni mahususi kusindikiza sherehe ya kumbukumbu za Mapinduzi ya Zanzibar yalianza Jana kwa mechi kati ya KVZ na Malindi.

Mechi zote za hatua ya makundi hadi nusu fainali zitachezwa Uwanja wa Amaan na fainali itapigwa Kisiwani Pemba katika Uwanja wa Gombani.



Chanzo: mwananchi.co.tz