Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam wapania taji la Ligi Kuu 

A9838c80fe999d8ea525eae16084862d.jpeg Azam wapania taji la Ligi Kuu 

Sat, 22 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BAADA ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United, Kocha Mkuu wa timu ya Azam FC, raia wa Zambia George Lwandamina, amesema kuwa bado yuko katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara licha ya kuzidiwa pointi moja na vinara Simba na Yanga.

Azam walipata mabao yao kupitia kwa mshambuliaji kiongozi Prince Dube, katika dakika ya 11 huku wakiongeza la pili katika dakika ya 54 kupitia kwa kiungo Mudathir Yahya .

Ushindi huo umeifanya Azam FC kufikisha pointi 60 baada ya michezo 30 lakini ikiendelea kusalia katika nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, pointi moja nyuma ya Simba na Yanga, ambao kila mmoja ana pointi 61.

Akizungumza na gazeti hili baada ya mchezo huo, Lwandamina alisema kuwa amefurahishwa na matokeo hayo, ambayo wameyapata katika mchezo huo yamewaongezea kasi katika mbio za kulisaka taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Ulikuwa mchezo muhimu kwetu katika mbio za ubingwa nashukuru tumepata matokeo mbele ya timu bora tulikuwa vizuri kila idara tulitengeneza nafasi, ambazo tumezitumia kupata matokeo,” alisema Lwandamina.

Naye Kocha Mkuu wa timu ya Biashara United, Patrick Odhiambo, alisema kuwa mchezo ulikuwa mzuri wameadhibiwa kutokana na makosa waliyofanya, lakini hiyo haiwezi kuwafanya wakakata tamaa katika mipango yao ya michezo ijayo ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

“Nawapongeza wapinzani wetu walikuwa bora ndio maana wamepata matokeo tunarudi kujipanga kurekebisha tulipokosea ili tusirudie makosa katika michezo inayofuata,” alisema Odhiambo.

Chanzo: www.habarileo.co.tz