Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam "Ugeni umetuondoa Kagame Cup"

F657e9ad57c655752a4e0b07649899d6.jpeg Azam "Ugeni umetuondoa Kagame Cup"

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

KOCHA wa Azam, Vivier Bahati amesema uchanga wa wachezaji wake ndio sababu ya kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Kagame.

Michuano ya Kagame inafanyika nchini na Azam ilifungwa juzi na Nyasa Bullets katika nusu fainali na kutoa nafasi kwa timu wageni kucheza fainali baada ya KMKM ya Zanzibar na Yanga nazo kutolewa.

Azam ilipoteza mchezo huo kwa mikwaju ya penalti 4-3 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika dakika 120.

Akizungumza na HabariLEO jana, Bahati alisema mchezo huo ulikuwa mzuri na vijana wake walipambana kwa kadri ya uwezo wao lakini uzoefu mdogo ulikuwa kikwazo.

“Nawapongeza wachezaji wangu, walicheza vizuri kwa dakika zote 120, ni makosa madogo ndio yalitugharimu ikiwamo uzoefu mdogo lakini nafurahi kushiriki michuano hii, tumejifunza vitu vingi ambavyo ni faida kwa wachezaji wetu,” alisema Bahati.

Kocha huyo alisema lengo lao lilikuwa ni kulibakisha taji hilo nchini lakini imeshindikana na wanarudi kujipanga kwa ajili ya msimu ujao.

Bahati alisema kutolewa kwao hana mtu yeyote wa kumlaumu sababu kila mmoja alitimiza majukumu yake inavyotakiwa isipokuwa kilicho wasumbua ni uzoefu wa wachezaji wao ikilinganishwa na walionao wapinzani wao Nyasa Bullets.

Azam sasa itacheza mechi ya kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya KMKM kwenye uwanja wa Azam Complex kesho, kabla ya fainali itakayozikutanisha Express na Nyasa Bullets.

Chanzo: www.habarileo.co.tz