Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC yasaka rekodi mbili Ligi Kuu

B65580f5d0e7811c7d5ee3f93cebdd51 Azam FC yasaka rekodi mbili Ligi Kuu

Wed, 22 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TIMU ya soka ya Azam FC imesema inasaka rekodi mbili katika michezo yake ya mwisho kwa ajili ya kusherehekea kumaliza msimu salama.

Msemaji wa Azam FC, Thabit Zakaria alisema rekodi ya kwanza watahakikisha wanaandika kesho kwa kupambana ili kushinda mchezo dhidi ya Mbeya City ukiwakumbusha msimu 2013/2014 walivyochukua ubingwa wa Ligi Kuu katika mchezo wa pili kutoka mwisho.

Zakaria alisema ukiachilia mbali kuwania nafasi ya pili, wanakumbuka mwaka huo wa ubingwa walicheza na Mbeya City na wakashinda na sasa wanakutana tena katika mchezo wa pili kutoka mwisho hivyo, watajitahidi washinde ili kutengeneza kumbukumbu nzuri ya kukutana.

Pia, mchezo wa mwisho wa Tanzania Prisons wanatarajiwa kukutana Julai 26, mwaka huu hivyo, ikibaki siku moja mbele wakikumbuka siku waliyopanda Ligi Kuu wakitoka Ligi Daraja la Kwanza Julai 27, 2008.

“Michezo yetu miwili iliyobaki kila mmoja ni muhimu kwa sababu sio vizuri kumaliza tukishuka kidogo hata kama hatutamaliza nafasi ya pili, kushinda ni muhimu kusaidia kutukumbusha matukio kadhaa ya kufurahisha,” alisema.

Alisema mchezo wao wa kupanda ligi kuu wa mwisho walikutana na Majimaji na wakashinda kwa hiyo wanataka washinde dhidi ya Prison kuendelea kuwa na kumbukumbu nzuri ya kumaliza msimu salama.

Tayari kikosi cha Azam kilichokuwa Iringa kimewasili Dar es Salaam kujiandaa na michezo hiyo.

Katika mchezo uliopita walilazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli kwenye Uwanja wa Samora

Chanzo: habarileo.co.tz