Dar es Salaam. Timu ya Simba imelazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Azam FC mchezo wa Ligi Kuu uliopigwa leo Jumatatu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam
Suluhu hiyo ni mwendelezo wa kikosi hicho cha Patrick Aussems ambacho kimekwama kupata matokeo mazuri katika mechi zake mbili. Huo ni mchezo wa pili mfululizo baada ya ule uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Kagera Sugar ambapo timu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi ilifungwa bao 1-0.
Baada ya mchezo huo wa leo, Simba wapo kileleni wakiwa na alama 82, huku wakifukuzana na watani zao Yanga waliopo nafasi ya pili wakiwa na alama 80. Lakini Simba wana faida kwa kuwa na michezo mingi zaidi wanayohitajika kukamilisha kwenye ratiba yao.
Katika kipindi cha kwanza timu hizo zilizishindwa kutambiana na kuzifanya kwenda mapumziko bila kuziona nyavu za mwenzake kila upande.
Washambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere walionekana kusumbua ngome ya Azam mara kwa mara hata hivyo safu ya ulinzi ya Azam ilionekanaa kuwa imara.
Wakati ligi hiyo ikielekea ukingoni, Kagere anaongoza kwenye wafungaji akiwa na mabao 20 huku Okwi hadi sasa akiwa na mabao 14.
Pia Soma
- Tamasha la filamu la Cannes kujaa nyota wa muziki,
- Raptors yatinga fainali NBA Kanda ya Magharibi
- Guardiola aivulia kofia Liverpool