Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam FC kutetea ubingwa Kagame leo

67708 Pic+azam

Mon, 22 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Azam FC leo itakuwa na kibarua cha kuvunja rekodi ya AFC Leopards ya Kenya ambao wamewahi kutwaa kombe la Kagame mara tatu mfululizo, watakapocheza na KCCA.

Leopards walichukua kombe hilo kuanzia 1982 hadi 1984, huku Azam FC wakilichukua mwaka 2016 na 2018, na wanatarajia kuweka rekodi nyingine baada ya kutinga fainali msimu huu.

Azam walitinga fainali hiyo baada ya kuifunga Maniema kwa mikwaju ya penalti 5-4, huku KCCA ya Uganda wakiifunga Green Eagles 4-3 katika michezo ya nusu fainali.

Katika mechi za awali, Azam FC inayofundishwa na Etienne Ndayiragijje ilimaliza na pointi nne kundi B kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Mukura Victory, ikafungwa 1-0 na KCCA, ikatoka sare ya bila kufungana na Bandari FC kisha wakaifunga TP Mazembe 2-0 katika nusu fainali.

Akizungumzia mchezo wa fainali, winga machachari wa timu hiyo, Idd Kipagwile alisema wanatambua kwamba KCCA ni timu nzuri, lakini hawatakubali kuona kombe wanaloshikilia likiondoka.

“Unajua hawa jamaa walitufunga katika mchezo wa nyuma, hilo jambo hatutaki litokee mara mbili, wana timu nzuri lakini hii ni fainali lazima tupambane,” alisema.

Pia Soma

Kiungo Masoud Abdallah ‘Cabaye’, alisema wanaamini mwalimu wao atawapa mbinu za kuibuka na ushindi.

Chanzo: mwananchi.co.tz