Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Azam, Biashara United mechi ya viwango Bara

League Ed2 Azam, Biashara United mechi ya viwango Bara

Thu, 20 May 2021 Chanzo: ippmedia.com

Azam FC ambayo imerejea katika makali yake, itashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kuichapa KMC FC mabao 2-1, ikiwa ni kulipa kisasi cha kufungwa bao 1-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza.

Akizungumza na gazeti hili jijini, Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, alisema kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mechi hiyo na wamejipanga kuingia dimbani kusaka pointi tatu muhimu na kujiweka katika mazingira mazuri katika msimamo wa ligi hiyo.

Vivier alisema wanahitaji kuwakaribia vigogo wa soka nchini, Simba na Yanga ambao wako katika nafasi za juu.

Alisema kuelekea mchezo huo hakuna majeruhi na suala la nani atacheza litabaki kuwa huru na Kocha Mkuu, George Lwandamina atapanga kikosi chake kwa amani.

"Biashara United ni timu nzuri na wako vizuri, tumeshafanyia kazi ubora na mapungufu yao na tayari wameshafanyia kazi na wako tayari kwa ajili ya kutafuta pointi tatu muhimu."

"Malengo yetu ni kuhakikisha tunatafuta pointi tatu muhimu ili kujiweka katika nafasi nzuri katika mbio za kupambana na walikuwa juu yetu," alisema Vivier.

Azam FC iko katika nafasi ya tatu imekusanya pointi 57 na kucheza mechi 29, inakutana na Biashara United iliyo kwenye nafasi ya nne na wamejikusanyia pointi 45 baada ya kushuka dimbani mara 29.

Mechi nyingine ya ligi hiyo itakayochezwa leo kwenye Uwanja wa Highland Estates itakuwa ni kati ya wenyeji Ihefu SC dhidi ya Dodoma Jiji kutoka jijini Dodoma.

Chanzo: ippmedia.com