Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aussems filamu inaendelea Simba

86455 Pic+ausem Aussems filamu inaendelea Simba

Fri, 29 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hatima ya Kocha Patrick Aussems klabuni Simba sasa inasubiri uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya Klabu utakaokabidhiwa leo saa 11 jioni ripoti ya yale yaliyoafikiwa katika kikao cha Bodi ya Klabu kilichofanyika jana Alhamisi jioni.

Aussems alisimamishwa kwa muda wa siku tano tangu baada ya mechi yao ya Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting na alihudhuria kujitetea kwenye kikao hicho cha jana kabla ya uamuzi wa kuachana naye kutokana na kosa la kuondoka nchini kinyemela kwenda Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani zilizothibitishwa na baadhi ya wajumbe wa bodi ya Simba, kikao cha jana kiliendeshwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Moses Kaluwa akiwa sambamba na Mwanasheria wa klabu Michael Mhina na Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa.

Pia wengine walioshiriki kikao hicho ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa Bodi ya klabu ya Simba na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Barbara Harnandez na Kaimu Mwenyekiti wa Simba, Mwina Kaduguda. Mo Dewji mwenyewe hakushiriki kikao hicho.

Chanzo: mwananchi.co.tz