Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aussems aiweka Simba gizani

84958 Kocha+pic Aussems aiweka Simba gizani

Thu, 21 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kocha wa Simba Patrick Aussems ameibua sintofahamu baada ya kuondoka nchini katika mazingira ya kutatanisha.

Aussems aliwashitua viongozi wa klabu hiyo alipowaaga ghafla Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam, juzi alfajiri.

Jana asubuhi Simba ilifanya mazoezi kwenye viwanja vya Gymkhana Dar es Salaam chini ya kocha msaidizi Denis Kitambi.

Mtendaji Mkuu wa Simba Senzo Mazingisa alisema kocha huyo atarejea baada ya siku tatu atakapomaliza matatizo binfasi.

“Hatukuwa tunajua kama ana matatizo alituaga alipofika uwanja wa ndege anaondoka atarudi baada ya siku tatu,”alisema Mazingisa.

Kitendo cha Aussems kuondoka katika mazingira hayo kinaonyesha hali si shwari baina ya viongozi na kocha huyo raia wa Ubelgiji.

Tangu kuanza Ligi Kuu Tanzania Bara, Aussems alionekana kutokuwa na maisha marefu ndani ya klabu hiyo baada ya kuibuka madai ya uwezo wake kufikia kikomo.

“Simba imeshindwa kukubaliana na kocha kuhusu nidhamu mbovu ya wachezaji na kiwango cha uchezaji kimeshuka tangu kuanza msimu huu,”kilisema chanzo cha karibu ndani ya klabu hiyo.

Aussems ameondoka timu hiyo ikiwa kileleni katika ligi ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi tisa ikiwa imefungwa moja na msimu uliopita aliifikisha Simba robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Wakati Aussems akiondoka, habari za ndani zilisema Simba ipo mbioni kumrudisha kocha wa zamani Mfaransa Pierre Lechantre.

Aussems ameondoka Simba siku chache baada ya watani wao wa jadi Yanga kumtimua aliyekuwa kocha wake raia wa DR Congo Mwinyi Zahera.

Imeandikwa na Khatimu Naheka, Charles Abel na Thobias Sebastian

Chanzo: mwananchi.co.tz