Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askari Magereza achota mamilioni SportPesa

72973 Magerezapic

Mon, 26 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Askari wa Jeshi la Magereza Tanzania, Magabe Matiku Marwa kutoka Mugumu, Serengeti mkoa wa Mara na mtumishi wa Umma, Kingsley Pascal kutoka Biharamulo, Kagera wamevuna kitita cha Sh825 milioni baada ya kushinda poromosheni ya Jackpot inayoendeshwa na kampuni ya ubashiri wa matokeo ya michezo ya SportPesa.

Wawili hao wameweza kubashiri kwa usahihi matokeo ya mechi 13 za soka za ligi mbalimbali zilizochezwa wiki iliyopita.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Agosti 26,2019 Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas amesema kuwa wawili hao watagawana sawa fungu hilo la fedha ambalo pia litakatwa kodi.

"Tumewaita kuwajulisha kwamba Jackpot ya Sh825 milioni imeliwa na hao Watanzania wawili. Wawili hao kila mmoja atapata takribani Sh412 milioni na kodi ambayo watakatwa ni takribani Sh165 milioni,” amesema

Lakini kingine kinachovutia zaidi kwa Jackpot, tangu tumeanza kuitoa, tumeshalipa Sh4.4 bilioni. Ina maana kila wiki, Watanzania wamekuwa wakipokea mamilioni ya fedha na kubadili maisha yao," alisema Tarimba.

Kwa mujibu wa Tarimba, mbali na Sh825 milioni, kwa wiki hii SportPesa imetoa takribani Sh997 milioni ikiwa ni jumla ya fedha za Jackpot hiyo na fedha za bonasi kwa washindi wengine

Pia Soma



Chanzo: mwananchi.co.tz