Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal yatakata Emirates bila Sanchez yaiuwa Palace

1644 Arse TZW

Mon, 22 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Ligi kuu ya England imeendelea hii leo kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja mbalimbali huko Emirates klabu ya Arsenal imeweza kuchomoza na ushindi mnono wa mabao 4 – 1 bila mshambuliaji wake raia wa Chile Alexis Sanchez ambaye yupo mbioni kujiunga na Manchester United.

Wachezaji waliyokuwa mwiba katika mechi hiyo ni Monreal  akiiyandikia The Gunners bao la mapema kabisa dakika ya 6 kabla ya Iwobi kutupia dakika ya 10, Koscielny na Lacazette kila mmoja akishindilia msumari wa moto kwa Crystal Palace na kuifanya timu hiyo kupoteana kabisa uwanjani.

Kwa matokeo hayo Arsenal anakuwa na pointi 42 ikishika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ya England huku wakiwa wamecheza michezo 24.

Chanzo: bongo5.com