Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Arsenal imeshindwa kubakiza point tatu Emirates vs Liverpool

Sat, 23 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Ligi Kuu England msimu wa 2017/2018 imeendelea tena usiku wa December 22 2017 kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa Emirates, club ya Arsenal ilikuwa mwenyeji wa Liverpool katika uwanja wa Emirates usiku wa December 22 kucheza mchezo wao 19 wa EPL.

Arsenal ndio walikuwa nyumbani lakini hadi kufikia dakika ya 52 walikuwa nyuma kwa magoli mawili yaliyokuwa yamefungwa na Philipp Coutinho dakika ya 26 na Mohamed Salah dakika ya 52, upepo ulibadilika kuanzia dakika ya 53 Alex Sanchez alipofunga goli la kwanza kwa Arsenal.

Granit Xhaka alifunga goli la pili dakika ya 56 na Mesut Ozil akafunga goli la tatu dakika ya 58, kujisahau kwa Arsenal kuliwafanya Liverpool wasawazishe goli dakika ya 72 kupitia kwa Roberto Firmino na kuufanya mchezo kumalizika kwa kufungana magoli 3-3.

Msimamo wa EPL baada ya game ya Arsenal vs Liverpool kumalizika kwa kufungana magoli 3-3 #MillardAyoUPDATES pic.twitter.com/HLw1ukG1TT

— AyoTV (@AyoTV) December 22, 2017

“Nimeumia kuliko siku zote toka nimeanza kazi Simba”-Haji Manara

Chanzo: millardayo.com