Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Antonio Brown aachiwa kwa Dhamana

Antonio Brown 12 13 Gettyimages Ftr Eqx0it7s17n11rikcaecz6vkp Antonio Brown

Wed, 18 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya mchezaji wa zamani wa NFL, Antonio Brown, kukamatwa na kuwekwa jela toka Jumapili ya wiki iliyopita kwa kosa la kutolipa pesa ya matumizi kwa watoto wake, hatimaye ameachiwa huru kwa dhamana.

Inaeleza kuwa Wiltrice Jackson ambaye ni mzazi mwenzie mchezaji huyo alifungua mashitaka na kutaka akamatwe kutokana na kutojitambua huku akieleza kuwa Brown anadaiwa zaidi ya $30,000 za malezi ya mtoto.

Hata hivyo kutokana na kuachiwa kwake Polisi katika jimbo hilo wameeleza kuwa Brown aliachiliwa baada ya kutoa dhamana ya $15,000 ambayo ni zaidi ya tsh 37 milioni. Wawili hao wana mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 12 aitwaye Antanyiah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live