Sun, 8 Apr 2018
Chanzo: bongo5.com
Promota, Eddie Hearn ambaye anamsimamia bingwa wa uzito wa juu duniani, Anthony Joshua amesema kuwa bondia huyo kwa sasa anahitaji kupambana na Deontay Wilder au Alexander Povetkin.
Hearn amesema kuwa majadiliano tayari yameshaanza kati ya bondia wake Joshua dhidi ya bingwa huyo wa WBC, king Wilder, huku mjadala ukiendelea Povetkin.
Promota huyo amekiambia chombo cha habari cha Sky Sports, Dirisha la majadiliano lipo wazi kwa siku 30 hatua hiyo itakuwa nzuri kwa Anthony kujua nani atapigana nae kati ya Wilder au Povetkin.
Chanzo: bongo5.com