Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amunike atatupeleka Cameroon 2019?

11630 Pic+amunike TanzaniaWeb

Mon, 13 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Miaka 30 baada ya Mendonca kuachana na Barcelona, hatimaye staa wa Nigeria, Emmanuel Amunike aliweka rekodi ya kuwa Mwafrika wa pili kuvaa jezi ya Barcelona.

Aliivaa jezi hiyo kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2000, kwanza chini ya kocha wa Kiingereza marehemu, Sir Bobby Robson kisha chini ya kocha maarufu wa Kidachi, Louis van Gaal. Alitwaa mataji sita na Barcelona katika kipindi chake cha miaka minne klabuni hapo.

Leo hii Amunike amepewa kazi kubwa Tanzania kwa ajili ya kuiandaa na kuifikisha Fainali za Afrika mwakani, Taifa Stars zitakazofanyika nchini Cameroon.

Amunike ameingia mkataba wa miaka mwiwili na atakuwa na kazi ya kunoa pia timu za vijana za U-17, U-20 na U-23.

Enzi za Amunike

Enzi zake Winga huyo mwenye miaka 47 aliyeichezea Super Eagles mechi 27 na kufunga mabao tisa kati ya mwaka 1993–2001 alijitosa kwenye ukocha mwaka 2008 akiwa kocha msaidizi wa klabu ya Al Hazm. Baadaye aliteuliwa kuwa Kocha mkuu wa Julius Berger ya Nigeria aliyoinoa kwa muda mfupi kabla yam waka 2009–2011 kuinoa Ocean Boys, mwaka 2014-2017 aliinoa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Nigeria na 2017–2018 aliinoa klabu ya Al Khartoum SC ya Sudan.

Kocha wa 11

Amunike anakuwa kocha wa 11 kuinoa Taifa Stars ndani ya miaka 16, akitanguliwa na Mshindo Msolla, Tanzania (2002–03), Badru Hafidh, Tanzania (2003–06) na Júlio César Leal, Brazil mwaka 2006.

Mwingine ni Márcio Máximo, Brazil (2006–10), Jan Poulsen, Denmark (2010–12) Kim Poulsen Denmark (2012–14), Salum Madadi (2014, kocha wa muda), Mart Nooij, Uholanzi (2014–2015), Charles Boniface Mkwasa, Tanzania (2015–2017) na Salum Mayanga ambaye ni Tanzania

(2017) na 2018 Amunike kutoka Nigeria.

Mzaliwa huyu wa Eziobodo, Nigeria, hakupata mafanikio sana kiuchezaji katika medani ya kimataifa kwani aliiwakilisha Nigeria kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994, miaka Club career kwa ngazi ya klabu alianza kuwika akiichezea Julius Berger F.C ya kwao Nigeria kabla ya kuhamia Zamalek ya Misri mwaka 1994.

Kufanya kwake vizuri katika mchezo mmoja aliocheza wa fainali za Kombe la Dunia kukampa ulaji Sporting Clube ya Ureno alikofunga mabao saba katika msimu wake wa kwanza, bao

lililompa heshima ni alilofunga dhidi ya mahasimu wa jiji la Lisbon, timu ya Benfica katika ushindi wa 1–0 mchezo wa Desemba mosi 1994.

Desemba mwaka 1996 alisajiliwa na FC Barcelona kwa ada ya dola 3.6 milioni, katika

klabu hiyo licha ya kuanza vizuri hakupata mafanikio sana kwani aliumia goti lililomuweka nje kwa msimu mzima na mwaka 1997 klabu hiyo ikamtibia hadi mwaka 2000 ilipoamua kumuacha.

Baada ya kuondoka Barcelona alisajiliwa na Albacete Balompié pia ya Ligi Kuu Hispania lakini nako hakucheza sana kutokana na tatizo la goti ambako aliuzwa kwenda Busan I’Cons ya Korea Kusini, lakini alicheza kwa muda mfupi na kujiunga na Al-Wehdat SC ya Jordan, kabla ya goti hilo kumlazimisha kustaafu mwaka 2008.

Baada ya kustaafu aligeukia ukocha na akateuliwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya Al-Hazm ya Saudi Arabia, lakini miezi michache baadaye aliiac ha baada ya kupokea ofa ya kuwa skauti wa timu ya Manchester United.

Hakufanya kazi ya uskauti kwa kipindi kirefu kwani Desemba 23, 2008, Amunike aliteuliwa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Julius Berger, licha ya United kumkubalia kufanya kazi zote kwa pamoja lakini aliamua kuchana na uskauti na kubakia kwenye ukocha.

Chanzo: mwananchi.co.tz