Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amunike: Uzoefu umetugharimu Afcon

64727 PIC+AMUNIKE

Fri, 28 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KOCHA Mkuu Taifa Stars, Emmanuel Amunike amesema uzoefu mdogo kwa wachezaji wake ndiyo sababu kubwa ya kupokea kipigo cha pili kutoka timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars'.

Stars jana usiku ilijikuta katika wakati mgumu baada ya kupigwa bao 3-2 na Harambee Stars katika mechi ya Fainali za Afcon zinazofanyika jijini Cairo, Misri.

Amunike amesema kitendo cha timu yake kushindwa kulinda ushindi licha ya kuongoza mara mbili inatokana na uzoefu mdogo.

Amesema matokeo ambayo Stars imeyapata katika mchezo dhidi ya Harambee Stars yanaonyesha kwamba bado kuna safari ndefu ya kujenga wachezaji bora.

Amesema kwasasa kazi kubwa inatakiwa kuanzia kuzalisha vipaji sahihi watakaokuja kuwa  wachezaji wenye ubora kwa Taifa Stars wakiungana na wachache wenye uzoefu.

Kocha huyo Mnigeria amesema pia matokeo waliyoyapata sasa yameongeza kitu kwa wachezaji wake ambao wote ni fainali zao za kwanza.

Pia Soma

Amesema kama Stars itarudi tena kwenye mashindano kama hayo itakuwa na ubora tofauti wa kuweza kushindana tofauti na ilivyofanya sasa

Chanzo: mwananchi.co.tz