Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Amsha amsha Russia 2018

9310 AMSHAAAA TZW

Sat, 16 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

HUU sasa ndio utamu wa Kombe la Dunia kama ulikuwa hujui, inakusanya watu kibao kutoka pande zote za dunia.

Kwa mashabiki wapenzi wa soka na hata wale wengine ambao si wapenzi wa mchezo huo, wamekuwa wakizitumia fainali za Kombe la Dunia kama mtoko wa kwenda kufurahia maisha.

Huko Russia kumenoga kweli kweli. Imekuwa kawaida tu kwa mitaani kukutana na kundi moja badala la jingine la mashabiki na utaweza kuwatambua kutokana na bendera watakazokuwa wakipeperusha kwa wakati huo. Soka inawaleta pamoja watu wengi kweli kweli, kutoka mataifa ya mbali sana. Wote wapo Russia kwa sasa kufurahia Kombe la Dunia, kumenoga kinoma.

Jana Alhamisi ilipigwa mechi ya kwanza kwenye fainali hizo za Kombe la Dunia na leo Ijumaa zitapigwa mechi tatu, mwendo utakaozidi kupamba kasi hadi itakapofika fainali Julai 15.

Chanzo: mwananchi.co.tz