Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alliance yapambana kubaki Ligi Kuu kuziona Simba, Yanga

56292 Pic+allaiance

Wed, 8 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

MWANZA. VITA ya kushuka daraja inaendelea kuzipa presha timu za Ligi Kuu, ambapo Alliance FC imesema ili kuwa na matumaini ya kubaki kwenye Ligi hiyo msimu ujao ni kushinda mchezo wa kesho Alhamisi dhidi ya Mwadui FC.

Simba na Yanga zimeendelea kuwa kwenye vita ya ubingwa wa Ligi Kuu ambapo mchezo wa leo wa Simba dhidi ya Coastal Union utaamua nani atakuwa kileleni.

Alliance ambao ni msimu wake wa kwanza kushiriki Ligi Kuu,imekusanya pointi 38 na kukaa nafasi ya 17,ambapo Mwadui wamevuna alama 37 na kukaa nafasi ya 18.

Mchezo baina ya timu hizo ambao utapigwa kwenye uwanja wa Nyamagana jijini hapa,ambapo kila upande utahitaji ushindi ili kujinasua nafasi za mkiani na kujiweka mazingira mazuri ya kukwepa kushuka Daraja.

Hata hivyo Mwadui inawavaa wapinzani hao ikiwa na rekodi nzuri kwani mchezo wao wa mzunguko wa kwanza uliopigwa mkoani Shinyanga,Alliance ilidundwa mabao 4-0.

Kocha Mkuu wa timu hiyo,Malale Hamsini alisema hali si shwari kwao hivyo matumaini ya kubaki kwenye Ligi msimu ujao ni kushinda mchezo wa leo dhidi ya Mwadui.

Alikiri mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar nyota wake kucheza chini ya kiwango na kueleza sababu kuwa walipania sana kushinda,jambo ambalo liliwakosesha pointi tatu na kuambulia sare ya mabao 2-2.

“Ni mchezo mwingine mgumu lakini muhimu sana kwetu,ushindi kwenye mechi hiyo ndio itatupa mwanga wa kubaki kwenye Ligi vinginevyo tutapaswa kuongea mengine”alisema Hamsini.

Kocha Mkuu wa Mwadui,Ally Bizimungu alisema baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya KMC waliolala mabao 2-0 sasa nguvu zote ni kwa Alliance kuhakikisha wanashinda.

“Kikosi kipo vizuri tunasubiri mchezo huo kuhakikisha tunashinda ili kujinasua nafasi za chini,tunaamini mechi itakuwa ngumu lakini tutapambana”alisema Bizimungu.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz