Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alliance wala hawana presha na Yanga wapata dawa ya Makambo

49224 Alliance+pic

Thu, 28 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Wakati Yanga wakiwasili leo asubuhi jijini Mwanza, Benchi la Ufundi la Alliance FC limesema wamegundua mbinu za kuwazima wapinzani hao katika mchezo wa kesho Jumamosi katika mchezo wa Kombe la FA.

Mchezo huo wa Robo fainali unatarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Kirumba jijini hapa huku Alliance ikiwa na lengo la kulipa kisasi kwa Yanga.

Katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu uliopigwa kwenye uwanja huo Yanga iliwatandika Alliance bao 1-0 lililofungwa na Amiss Tambwe dakika ya 75.

Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Kessy Mzirai alisema kwa sasa wapo katika mazoezi makali kuelekea mchezo huo hawataki kukubali kufungwa kwa mara ya pili.

Alisema nguvu zao wamezielekeza katika safu yao ya ulinzi ambayo inanolewa vilivyo ili kuweza kuwathibiti washambuliaji wa Yanga wanaongozwa na Heritier Makambo.

“Ule mchezo uliopita ulitupa somo kubwa la kuwajua Yanga sasa tupo kwenye mazoezi kikubwa tunalenga kuhakikisha hawatufungi na sisi tunawashambulia mwanzo mwisho huku tukilinda lango letu”alisema Mzirai.

Kocha huyo alisema wanajua ugumu wa mchezo huo lakini nao msimu huu wamejipanga kuhakikisha wanafika Fainali ya Kombe hilo na hatimaye kunyakuwa ubingwa na kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya Kimataifa.

“Tunatamani na sisi kushiriki mashindano ya kimataifa na sehemu yenyewe ambayo tukitaka tufikie hayo mafanikio ni kwenye hili Kombe la FA hivyo tutapambana hadi haya malengo yetu kukamilika,”alisema Kocha huyo.



Chanzo: mwananchi.co.tz