Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alliance, Mwadui vitani Ligi Kuu Bara

56445 ALLIANCE+PIC

Thu, 9 May 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Wakati vita ya kushuka daraja ikiendelea kuzipa presha timu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, Kocha wa Alliance, Malale Hamsini amesema mchezo wa leo dhidi ya Mwadui ya Shinyanga utakuwa ni vita.

Akizungumza jana, Hamsini alisema Alliance inapaswa kushinda mchezo ili kubaki katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alliance yenye pointi 38 ikiwa nafasi ya 17 kama ilivyokuwa Mwadui iliyovuna pointi 37 na ipo nafasi ya 18, zipo katika hatari ya kuteremka daraja endapo zitashindwa kucheza vyema karata zao katika mechi zao zilizobaki.

Nyasi za Uwanja wa Nyamagana, Mwanza zinatarajiwa kuwaka moto leo wakati timu hizo zitakapoteremka uwanjani kuwania pointi tatu muhimu.

Hamsini alidai hatakubali kufungwa kwa mara nyingine katika mchezo huo kama ilivyotokea mechi ya mzunguko wa kwanza waliofungwa mabao 4-0.

Alisema mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar wachezaji wake walicheza chini ya kiwango tofauti na maelekezo ya benchi la ufundi na ndiyo sababu ya kupata sare ya mabao 2-2.

Kocha wa Mwadui Ally Bizimungu alisema baada ya kufungwa na KMC mabao 2-0, akili zao wameelekeza katika mechi dhidi ya Alliance.

“Kikosi kipo vizuri. lengo letu ni kuhakikisha tunashinda tutoke latika nafasi za chini,” alisema Bizimungu.



Chanzo: mwananchi.co.tz