Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyekuwa kocha wa makipa Yanga Pondamali afunguka alivyoomba kuachwa

86176 Pic+pondamali Aliyekuwa kocha wa makipa Yanga Pondamali afunguka alivyoomba kuachwa

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

ALIYEKUWA kocha makipa wa Yanga, Juma Pondamali 'Mensah' amefunguka kuwa si aliomba kuacha kazi mwenyewe ya kuwanoa makipa hao kutokana na mambo aliyokuwa akiyaona mbele. Pondamali alisema kwanza kabla ya msimu kuisha iliona tukio la wapenzi wa Yanga nchi nzima kuichangia timu hiyo kwa maana yake msimu huu ukianza walitakiwa kuchukuwa ubingwa wa ligi na kufanya vizuri kwenye mashindano mengine jambo ambalo lisingekuwa rahisi. "Baada ya uongozi wa Mwenyekiti Mshindo Msola, kuingia madarakani nilimfuata na kumuuliza mipango yetu ya msimu ujao ndani ya kikosi ikoje alinijibu kuwa wale wachezaji ambao tutaachana nao tutawapa stahiki zao zote haraka na mapema lakini wale ambao tutabaki nao tutawapa siku za mbele taratibu," "Kutoka moyoni mwangu nilimuomba Msola kuwemo katika orodha ya hao watakaoachwa ili nipate stahiki zangu zote kwa wakati kuliko kuendelea kubaki,  si kama niliondoka kwa kupewa barua. "Baada ya kukubalina na Msola, niliondoka ili nipate hizo stahiki zangu, maamuzi hayo ni baada ya kuona timu inakoelekea haiwezi kufikia malengo yake na benchi lingetimuliwa kabla hata msimu haujamalizika jambo ambalo lilitokea baadaye. "Baada ya kuachana na Yanga wakati huu naendelea na shughuli zangu za kufanya muziki na nimeachia kibao kimoja kinaitwa 'Pesa', ambacho nina imani kitafanya vizuri kwani ni nyimbo nzuri," alisema Pondamali ambaye alilipwa kiasi tu cha pesa kwenye madai yake ambapo pia hakuweka wazi kiasi hicho.

Chanzo: mwananchi.co.tz