Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyeenguliwa urais TFF ateuliwa kamati tendaji

Tff Pic1 Data Aliyeenguliwa urais TFF ateuliwa kamati tendaji

Sat, 7 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Hawa Mniga ambaye alichukua fomu kugombea urais kwenye uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ameteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya utendaji.

Baada ya kuidhinishwa leo kuwa rais wa TFF kwa awamu ya pili, Wallace Karia amewateua wajumbe wanne kuingia kwenye kamati Tendaji akiwamo Mniga, ambaye alijitosa kuwania urais kwenye uchaguzi huo na kuenguliwa kwenye usaili kwa kukosa sifa ya uzoefu.

Mniga ni miongoni mwa wajumbe wanne walioteuliwa na rais saa chache baada ya zoezi la kumuidhimisha Karia kuendelea kuongoza Shirikisho hilo kufanyika mjini Tanga.

Wengine aliowateua ni Athuman Nyamlani ambaye alimteua pia kuwa makamu wa rais wa TFF kwa miaka minne ijayo.

Wajumbe wengine walioteuliwa na rais ni Ahmed Mgoyi na Said Sudi.

Imeandikwa na Raisa Said na Imani Makongoro

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz