Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alikiba aishudia Coastal Union jukwaani

15092 KIBA+PIC TanzaniaWeb

Sun, 2 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Mshambuliaji mpya wa Coastal Union, Ali Kiba ‘Kingkiba’, alikuwa jukwaani akishudia timu yake ikilazimishwa sare ya bao 1-1 na KMC kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Mamia ya mashabiki wa Coastal Union walijitokeza uwanjani hapo kwa nia ya kumuona Alikiba akicheza mechi yake ya kwanza na mabingwa hao wa mwaka 1988, walishia kumtazama akiwa jukwaani.

Katika mkataba wake na Coastal kutokana na kuridhia kuitumikia timu hiyo bila malipo mchezaji huyo anaruhusiwa kuondoka kambini na kwenda kufanya onyesho au kazi nyingine za kimuziki.

Hata hivyo Alikiba aliliambia Mwananchi kuwa anatarajia kuanza kuitumikia rasmi katika mchezo ujao, kwani ameshamaliza ziara za kimuziki zilizompeleka Marekani na Canada.

Timu hiyo bado haijatoka kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Mkwakwani tangu kuanza kwa Ligi hiyo Agosti 22 mwaka huu, jana ilifikisha pointi tano baada ya kucheza michezo mitatu ikishinda mmoja dhidi ya Biashara United ya Mara na sare dhidi ya Lipuli ya Iringa.

Bao lililowaongezea pointi moja Coastal katika mchezo lilifungwa katika dakika ya 34 na Hamisi Mustafa, ambalo liliwafanya kwenda mapumziko wakiongoza kwa 1-0.

Chanzo: mwananchi.co.tz