Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichoambiwa bondia Hassan Mwakinyo na Waziri Mkuu

17804 Pic+mwakinyo TanzaniaWeb

Mon, 17 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma, Ijumaa iliyopita, bondia Hassan Mwakinyo baada ya kutoka bungeni mjini hapa alikaribishwa nyumbani kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, pamoja na kuelezwa mambo mengi lakini jambo kubwa aliloambiwa ni kuungwa mkono na serikali ya awamu ya tano.

Akiwa kwa Waziri Mkuu, Mwakinyo aliahidiwa kupewa sapoti na serikali ambayo itakuwa naye bega kwa bega katika kuhakikisha anafika mbali zaidi na kukikuza kipaji chake.

Bondia huyo aliambiwa kuwa, serikali itamsaidia katika masuala yake ya kimkataba kila itakapohitajika kufanya hivyo.

Kutokana na hayo Waziri Mkuu amemtaka bondia huyo kuhakikisha anajiandaa vema kwa kufanya mazoezi ya nguvu wakati wote na sio kusubiri kufanya maandalizi ya zimamoto pale anapokabiliwa na pambano.

Mwakinyo aliyepanda katika viwango vya ubora hadi ya 16, alionyesha furaha baada ya maneno hayo na kuahidi kuhakikisha hawaangushi watanzania.

Ahadi hiyo ya serikali imetokana na Mwakinyo kumshinda kwa TKO raundi ya pili, Sam Eggington wa Uingereza katika pambano lisilo la ubingwa llilofanyika wikiendi iliyopita mjini Birmingham Uingereza, anatarajiwa kuwania taji la ubingwa dunia la IBF uzani wa kati.

Chanzo: mwananchi.co.tz