Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AliKiba aanza kukinukisha Coastal Union

10016 Pic+alikiba TanzaniaWeb

Sat, 4 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tanga. Mashabiki wa Coastal Union wamebaki midomo wazi baada ya kumuona msanii Ali Kiba akijiunga na wenzake moja kwa moja baada ya kutua katika mkoa huu.

AliKiba alikuja maalum kwaajili ya kukamilisha zoezi la sherehe ya mdogo wake Zabibu Kiba, aliyeolewa na Mchezaji Abdi Banda anayeichezea Baroka Fc ya nchini Afrika Kusini.

Msanii huyo hakuwa kivutio kwa mashabiki tu mazoezini hapo, bali hadi kwa upande wa wachezaji wenzake walionekana kumtaka awe fiti zaidi kama yeye.

Kiba katika mazoezi hayo alionekana kukubali kuelekezwa kila kitu na kocha wake Juma Mgunda, huku akiweka ustaa wake pembeni.

Mgunda alikuwa akiwafanyisha mazoezi ya kuchezea sana mpira hasa katika upande wa koni, na AliKiba alionekana kuliweza zoezi hilo vizuri.

Chanzo: mwananchi.co.tz