Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Al-Khelaifi afunguka juu ya hatma ya Mbappe PSG

Mbappe Al-Khelaifi afunguka juu ya hatma ya Mbappe PSG

Tue, 25 May 2021 Chanzo: eatv.tv

Mwenyekiti wa klabu ya PSG ya nchini Ufaransa, Nasser Al-Khelaifi amesema anaimani kubwa kuwa mshambuliaji wake nyota, Kylian Mbappe atasalia klabuni hapo licha ya kuwepo kwa fununu kuwa nyota huyo ananukia Real Madrid ya Hispania.

Akizungumza baada ya mchezo wa mwisho wakutamatisha ligi kuu ya Ufaransa ambao PSG waliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kuukosa ubingwa wa Ufaransa, Khelaifi amesema :

"Kylian ni mchezaji wa PSG, na ataendelea kuwa mchezaji wa PSG. Sina wasi wasi. Mbappe ni mfaransa na ni mtu halisi wa PSGm badi ana mkataba na sisi na anataka kusalia kwa 100%". 

Baada ya kusema hayo, Mbappe mwenye akafunguka kuhusu vitu anavyotaka viwepo PSG ili kumfanya asalie klabuni hapo:

"Ninataka kushinda, Ninataka kuona kuna mipango ya mafanikio hapa". Mbappe aliyasema hayo baada ya kupewa tuzo ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Ufaransa na mfungaji bora wa ligi hiyo kwa kufunga mabao 27 na kuchukua tuzo hiyo mara tatu mfululizo.  

Chanzo: eatv.tv