Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajibu anavyombeba Zahera, Makambo kimyakimya

32739 Pic+ajibu Tanzania Web Photo

Fri, 21 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mshambuliaji Ibrahim Ajib amebeba siri ya mafanikio ya kocha Mwinyi Zahera katika kikosi cha Yanga baada ya kuhusika katika mabao 16 kati ya 32 yaliyofungwa na vinara hao wa Ligi Kuu Bara.

Ajib msimu huu amefanikiwa kufunga mabao matano (5) na kutegeneza pasi za mwisho 11, zilizozaa mabao katika michezo kumi na saba iliyocheza timu yake.

Kwa mujibu wa takwimu zilizonazo Mwanaspoti, Ajib ametoa pasi 11 za mabao na kufunga mabao matano na kufanya kuwa mchezaji aliyetegeneza pasi nyingi zaidi za mwisho Ligi Kuu Bara hadi sasa.

Mshambuliaji, Heritier Makambo anayeongoza kwa ufungaji Yanga amefaidika zaidi na pasi za Ajibu

Katika mabao 9 aliyofunga Makambo goli matatu ni pasi za Ajibu jambo linalofanya Mkongo huyo kuwa hatari zaidi anapocheza pamoha na Ajibu.

Alifunga katika mchezo dhidi ya Yanga na Coastal Union ambapo Makambo ndiye aliyefunga bao pekee la ushindi akipokea pasi kutoka kwa Ajibu, katika mchezo na Alliance ambapo waliibuka na ushindi wa bao 3-0 pia katika mchezo dhidi ya Ruvu Shooting ambapo yanga iliibuka na ushindi wa bao 3-2.



Chanzo: mwananchi.co.tz