Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajib aanzia benchi Stars

68656 Pic+ajibu

Sun, 28 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib amejikuta akikaa benchi katika kikosi cha timu ya Taifa Tanzania, licha ya kurejeshwa katika kikosi hiko na kaimu kocha mkuu, Ettiene Ndayiragije.

Ajib aliitwa na kocha wa zamani wa stars, Emmanuel Amunikea katika kikosi kilichokuwa  kinajiandaa na mechi za kufuzu Stars, lakini aliondolewa kwa kile kinachodaiwa ni utovu wa nidhamu,

Hata hivyo katika kikosi cha Ndayiragije, Ajib pia licha ya kurejeshwa alijikuta akianzia benchi katika mchezo huo.

Wachezaji wengine ambao Ettiene amewarudisha, Jonas Mkude na Salum Aboubacary 'Sure Boy' wao walipata nafasi ya kuanza katika kikosi hiko.

Kikosi kilichoanza, Juma Kaseja, Paul Godfrey, Gadiel Michael, Kelvin Yondani, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Salum Aboubacary, Hassan Dilunga, Idd Seleman, John  Bocco na Ayoub Lyanga.

Chanzo: mwananchi.co.tz